You are here
Kimataifa 

Korea Kaskazini yatuma ujumbe kwa Trump huku ikitishia kurusha kombora la masafa marefu muda wowote

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na Rais Mteule wa Marekani Donald Trump.

(CNN)

KOREA Kaskazini imesema inaweza kurusha kombora la masafa marefu “muda wowote,” hata kama ilionekana kutoa nafasi ya baadae ya mazungumzo kwa Donald Trump.

Hali ya wasiwasi katika peninsula ya Korea imezidi kuongezeka tangu kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un aliposema katika ujumbe wa mwaka mpya kwamba nchi yake ilikuwa karibu kufanya majaribuo ya kombora la masafa marefu ambalo linauwezo wa kubeba silaha ya kinyuklia hadi Marekani.

Katika taarifa siku ya Jumapili, msemaji kutoka wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini alisema “Marekani inapaswa kulaumiwa” kwa mpango wake wa makombora.

Akizungumza na shirika la habari la NBC, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Ash Carter aliliita suala hilo kama “tishio kubwa” na alisema kwamba Marekani italitungua kombora lolote ambalo litakuwa limeelekezwa kwake au kwa mshirika wake.

China na Korea Kusini ziliishutumu tishio la kombora la Korea Kaskazini na zikaonya kwamba jaribuo hilo linaweza kusababisha vikwazo zaidi dhidi ya nchi hiyo.

“Iwapo Korea Kaskazini itadharau maonyo yetu na kurusha kombora la masafa marefu, itakabiliwa na vikwazo vikali zaidi na shinikizo kutoka kwa jamii ya kimataifa,” msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini Moon Sang-gyun alisema.

Uchaguzi kidogo

Vikwazo vya kimataifa vimeshindwa kuizuia Prongyang kuendeleza mpango wake wa kinyuklia.

Katika taarifa Jumapili, wizara ya ulinzi ya nchi hiyo alikwepa vikwazo hivyo na kusema maafisa wa Marekani “wanazungumza uchafu” wakati wanapodhania kwamba sera za Obama zinaendelea siku za usoni.

“Yeyote anayetaka kuzungumza na Korea Kaskazini anashauriwa kuwa na njia mpya ya kufikiri baada ya kuelewa,” taarifa hiyo ilisema.

John Deluru, Profesa msaidizi wa masomo ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Yonsei alisema kwamba taarifa hiyo “ni ujumbe kwa timu ya kubadilishana madaraka ya Trump kusema kwamba usifuate njia hii ya vikwazo.”

Trump kuzungumza?

Kufuatia tishio la wazi la Pyongyang la kutumia nyuklia katika hotuba yake ya mwaka mpya, Trump kwa kutumia Twitter alisema kwamba “Korea Kaskazini imesema kwamba ipo katika hatua za mwisho za kuuanza bomu la nyuklia ambalo lina uwezo wa kufika Marekani. Hilo halitatokea!”

Mshauri wa Trump Kellyanne Conway baadae aliulizwa ni kitu gani Rais Mteule Trump alikuwa amepanga kufanya kuzuia nyuklia za Korea Kaskazini. “Hajasema hadharani, na hatasema kabla hajaapishwa,” Conway alisema.

Wachambuzi wamesema kwamba Trump, kupitia matangazo yake mwenyewe na kushindwa kwa utawala wa Obama kuizuia Korea Kaskazini kuunda silaha za kinyuklia, amebaki na mambo machache kuweza kufanya.

Tangu mazungumzo ya pande sita yalipovunjika mwaka 2009, Korea Kaskazini inadai imefanya majaribio manne yaliyofanikiwa ya kinyuklia, na kuimarisha nguvu yake katika mazungumzo ya baadae.

“Korea Kaskazini inajaribu kumpa nafasi Trump kuacha sera za Obama na kuzungumza nao.”

Bruce Bennett, mchambuzi wa masuala ya kijeshi wa Rand Corporation, aliiambia CNN wiki iliyopita kwamba pamoja na maendeleo ya Korea Kaskazini katika silaha za kinyuklia, lakini bado haina teknolojia ya kutosha ya makombora na roketi yenye uwezo wa kubeba bomu la nyuklia.

Marekani imekuwa ikishirikiana na Korea Kusini katika kupeleka mfumo wa ulinzi wa anga wa THAAD nchini Korea Kusini, lakini bado haijajulikana kama utaendelea baada ya kuingia madarakani kwa Trump.

Mwandishi: Mwandishi Wetu kutoka Raia Mwema
Tembelea Chanzo

Related posts