You are here

DC Hapi aahidi kumaliza migogoro iliyoshindwa kutatuliwa Kamati ya Utatuzi Migogoro

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameanza kushughulikia kero nzito na sugu zilizoshindwa kutatuliwa na Kamati ya Utatuzi Migogoro ya wilaya hiyo.

Kupitia taarifa yake aliyoitoa leo kwa waandishi wa habari, DC Hapi amewataka wananchi walioporwa haki zao na kukosa msaada, kufika ofisini kwake kila siku ya jumatatu na alhamisi.

“Baada ya ziara yangu ya kazi kwenye kata zote 20 za Kinondoni iliyofuatiwa na mapumziko mafupi, sasa nimeanza kusikiliza wananchi wenye kero nzito na sugu ambazo kamati yangu ya utatuzi migogoro imeona kwa uzito huo inafaa ziletwe kwangu mwenyewe,” amesema na kuongeza.

“Kama umeporwa haki yako, umetapeliwa kiwanja chako, unanyanyaswa, unakandamizwa na yoyote na kwa unyonge wako kila unakoenda husaidiwi au unaona dalili za mkandamizaji, kupendelewa, njoo unione ofisini siku za jumanne na alhamisi,

“Najua wapo baadhi ya watu waliozoea kuishi kwa. utapeli, dhuluma au uporaji wa haki za wanyonge kwa kutumia ubabe au nguvu ya pesa.”

Aidha, amewatoa hofu wananchi wa Kinondoni katika upatikanaji wa haki zao kwa kuwa serikali iko pamoja nao.

“Niwatoe shaka wananchi wa Kinondoni kuwa serikali yenu ipo. Tutaendelea kuwashughulikia wote na kila mwenye haki haki yake haitapotea,” amesema.

Na Regina Mkonde

Mwandishi: Rabi Hume kutoka DEWJIBLOG

Related posts