You are here

Orodha ya Forbes ya wasanii wa Hip-Hop walioingiza mkwanja mrefu zaidi 2017 ‘Highest-Paid Hip-Hop Artist’

Jarida la Forbes limetoa list ya wasanii wa HIPHOP walioingiza mkwanja mrefu zaidi mwaka 2017 ‘Highest-Paid Hip-Hop Artist’ pesa hizo ni walizoingiza kuanzia mwezi agosti 2016 hadi agosti 2017.

Sean ‘Diddy’ Combs ameongoza orodha hiyo kwa kulipwa kiasi cha dola milioni 130 kwa miezi 12 iliyopita. Drake anafuata kwenye orodha hiyo akiwa amelipwa dola milioni 94.

Wakati huo huo Jay Z ambaye orodha iliyopita alishika namba mbili ameporomoka mpaka katika nafasi ya tatu akiwa amelipwa dola milioni 42 kwa mwaka huu. Hii ni orodha ya mastaa 10 walioongoza kulipwa zaidi.

1. Diddy
2. Drake
3. JAY-Z
4. Dr. Dre
5. Chance the Rapper
6. Kendrick Lamar
7. Wiz Khalifa
8. Pitbull
9. DJ Khaled
10. Future

Mwandishi: sadock kutoka TEAMTZ

Related posts