You are here

AFRIMA 2017: Alikiba na Nandy waibuka kideda, Kiba aondoka na tuzo mbili

Usiku wa kuamkia leo nchini Nigeria kulitolewa tuzo za All Africa Music Awards 2017 (AFRIMA) ambapo wasanii wawili kutoka Bongo, Alikiba na Nandy wameibuka washindi.

AFRMA1

Alikiba ameshinda Tuzo mbili katika vipengele vya Best Africa Collaboration kupitia ngoma ‘Aje’ pamoja na kipengele cha Best Artist or Group in Africa RnB and Soul ambapo pia ni kupitia ngoma ya ‘Aje’ kwa kushirikiana na M.I.

AFRIMA2

Wakati huo Nandy akishinda katika kipengele cha Best Female Artist In Eastern Africa Award. Wasanii wengine wa Tanzania waliokuwa wakiwania ni pamoja na Feza Kessy na Vanessa Mdee.

AFRIMA3

 

Mwandishi: sadock kutoka TEAMTZ

Related posts