You are here

Diamond ataja tarehe atakayoachia wimbo wake na Rick Ross na album yake mpya

Tarehe 1 mwezi wa Disemba ndio siku ambayo Diamond ataachia audio na video ya collabo yake na Rick Ross, Diamond amefunguka alipokuwa akihojiwa na BBC Swahili.

23347567_1220424938058095_4897752869228249088_n-1

Pia Boss huyo wa WCB amesema album yake ya ‘A Boy From Tandale’ yenye ngoma 18 itakuwa tayari kwa pre-orders siku hiyo hiyo huku akitaja baadhi ya wasanii aliowashirikisha kwenye album hiyo.

“Nimewashirikisha wasanii tofauti tofauti japo kuwa wengine naogopa kuwataja ili isife. Kuna msanii kama Young Killer nimefanya nae kutoka nyumbani Tanzania, Nigeria nimefanya na Davido. Wote watakuwepo kwenye albamu yangu hii mpya ‘A Boy From Tandale’,” amesema Diamond

 

Mwandishi: sadock kutoka TEAMTZ

Related posts