You are here
Burudani 

Msondo Ngoma kumshitaki daimond na kudai fidia ya Milioni 300

FB_IMG_1510460742690

– Diamond Platinumz atakiwa kulipa milioni 300 kwa kuiba wimbo
Bendi ya muziki nchini Tanzania ya Msondo Ngoma, imemtaka msanii wa muziki wa bongo fleva, Diamond Platinumz pamoja na kundi lake la Wasafi Classic Baby (WCB) liwalipe fidia kwa kuiga kionjo cha muziki uliopigwa katika nyimbo ya ‘Ajali’ bila idhini ya mmiliki.
Msondo Ngoma kupitia kampuni ya Mawakili ya Maxim imeitaka Wasafi Clasic Baby (WCB) kuwalipa fidia ya kiasi cha shilingi 300 milioni kutokana na kutumia kionjo hicho cha muziki kilichotungwa na kupigwa katika wimbo wao wa ‘Ajali’ na kukirudia katika wimbo wao wa ‘Zilipendwa’ bila kupata idhini ya mmiliki.
Kionjo hicho kilichotungwa na kupigwa kuanzia dakika ya 6:38 hadi 6:52 kwenye wimbo wa ‘Ajali’ mali ya Msondo Ngoma, kimeigwa na kupigwa katika wimbo wa ‘Zilipendwa’ kuanzia dakika ya 4:55 hadi 5:10.
Barua hiyo imeitaka WCB kulipa fedha hizo ndani ya muda wa siku saba na kama wakishindwa basi Msondo Ngoma watawachukulia hatua zaidi za kisheria.
WEWE UNAMAOI GANI

494 total views, 494 views today

The post Msondo Ngoma kumshitaki daimond na kudai fidia ya Milioni 300 appeared first on The Choice.

Mwandishi: choicetz kutoka The Choice

Related posts