You are here

Yemi Alade: Sarkodie ameninyima collabo mara tatu

Mwimbaji kutoka Nigeria Yemi Alade ameweka wazi masikitiko yake juu ya tabia ya msanii kutoka Ghana Sarkodie kumnyima Colabo kila mara.

Kwenye Interview Yemi Alade anasema “Naweza kuhesaba zaidi ya nchi tatu ambazo team yake imekutana na team yangu kuongelea swala la colabo, kila mara anakubali ila inapokuja kufanya kazi inakuwa ngumu sana kwake, sitaki kuleta swala la kwamba mimi ni mwanamke ndio maana anafanya hivyo, nimeshajenga jina langu kwahiyo sio tatizo sana ila hajawahi hata kuomba msamaha kwa mambo anayonifanyia, sio mwenendo mzuri wa kazi huu”.

Sarkodie, tayari amefanya colabo na wasanii wa Nigeria kama  Tiwa Savage ,Seyi Shay na Patoranking.

Yemi Alade anatoa album yake mpya Black Magic 15 December 2017

Mwandishi: sadock kutoka TEAMTZ

Related posts