You are here

Uongozi na wafanyakazi gazeti la Mwananachi wapaza sauti ya #BRINGBACKAZORY

Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania leo Desemba 7,2017 imetoa tamko la kuitaka Serikali na mamlaka zake kusaidia kupatikana kwa mwandishi wao wa kujitegemea wa gazeti hilo aliyekuwa akiripotia kutokea kwa muda wa siku 17, hadi leo.

Mkurugenzi wa gazeti la Mwananchi Francis Nanai akielezea mbele ya vyombo vya habari pamoja na uongozi na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa pamoja ambao walivaliamavazi meusi na mabango ya ‘BringBackAzory, waliungana kwa pamoja katika tukio hilo.

Nanai ameviomba  vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza juhudi za kumsaka Azory  kwa kutoweka kwake  kwa kipindi hicho cha zaidi ya siku 10.

“MCL ilipata taarifa za kupotea kwa Azory  tokea  Novemba 30,mwaka huu kutoka kwa ndugu zake na Mkewe. Tumefuatilia tukio hilo kwa vyombo vyote vya Ulinzi na mpaka leo hatujapata taarifa. Juhudi za kufuatilia zinaendelea kwa kutoa habari kwa vyombo vya ndani na nje. Pia tunaendelea kufanya hivyo huku pia tukiendelea kumfariji mkewe.

Pamoja na hayo, MCL imeandika barua kwa Waziri wa Habari, Spika wa bunge,TEF, MCT, Vitukio vya sheria na haki za Binadamu na wadau wengine kuhusu kupotea kwa mwandishi wetu” alieleza Nanai.

Imeelezwa kuwa, Azory alianza kulitumikia gazeti hilo kama mwandishi wa kujitegemea kuanzia 2015 mpaka sasa kutoweka kwake.

Nanai  amebainisha kuwa, kwa kuwa hawajui ameshikiriwa na nani ama kwa kosa gani, wanaomba kumpata mwenzao akiwa hai mazima na mwenye afya njema ili waungane nae katika majukumu yake ya kila siku.” Alieleza Nanai katika taarifa yake hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti ya jukwaa la wahariri Teofile Makunga ambaye aliungana na MCL, aliomba mwandishi huyo kama anashikiliwa na watu basi aachiwe ama apelekwe mahakamani.

“Kama mwenzetu ameshikiliwa na vyombo vya usalama kwa sababu yoyote angetakiwa kuwa amefikishwa mahakamani kufikia sasa. Lakini kwa kimya hiki cha siku 17, zinatia mashaka na kutishia tasnia ya habari hapa nchini”alieleza Makunga.

Hata hivyo, tayari wadau wa habari wanatarajia kufanya maandamano ya kushinikiza kuzidishwa kazi kwa msako huo yatakayoanzia mnazi mmoja hadi makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani jijini Dar es Salaam kwa nia ya kufikisha ujumbe kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro.

Na Andrew Chale,MO BLOG

Mwandishi: Andrew Chale kutoka DEWJIBLOG

Related posts