You are here
Burudani 

BEBE COOL: WATOTO SITA HAWANITOSHI

KAMPALA, UGANDA NYOTA wa muziki nchini Uganda, Bebe Cool, baada ya wiki iliyopita kuthibitisha kuwa amepata mtoto wa sita, sasa amesema watoto hao hawatoshi katika maisha yake. Msanii huyo ambaye alifanikiwa kufunga ndoa na mpenzi wake, Zuena Kirima, kwa miaka 14 iliyopita, amesema lengo lake ni kuwa na familia kubwa na yenye furaha. “Nashukuru Mungu kwa kutuongezea ukubwa wa familia yetu, lengo la familia yetu ni kuwa kubwa na tunaamini kwa uwezo wake Mungu tutafanikiwa kama tulivyopanga. “Kwa sasa nina jumla ya watoto sita, lakini bado hawanitoshi, natamani kuwa na…

Read More
Burudani 

T-PAIN: MKATABA UNAMPA WAKATI MGUMU

NEW YORK, MAREKANI RAPA T-Pain ameweka wazi kuwa anashindwa kuachia nyimbo mara kwa mara kutokana na kubanwa na mkataba wake chini ya lebo ya RCA. Msanii huyo amesema tayari ana nyimbo nyingi ambazo ameziandaa, lakini kutokana na mkataba wake unavyosema, anashindwa kuwapa burudani mashabiki wake. “Nimekuwa kimya kwa muda mrefu sana, si kama kazi hazipo hapana, zipo nyingi sana ila mkataba wangu unataka nitoe kazi kwa muda fulani, nimewamisi sana mashabiki zangu. “Niwaondoe wasiwasi kwamba baada ya miezi sita kuanzia sasa kazi zangu zitaanza kusikika, hivyo mashabiki wakae tayari kwa…

Read More
Burudani 

SHILOLE AWAJIBU WANAOIPONDA NDOA YAKE

Na ESTHER GEOR-DAR ES SALAAM MSANII wa muziki nchini Tanzania, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, amefunguka na kusema wanaoiponda ndoa yake kwenye mitandao ya kijamii wana chuki binafsi. Akizungumza na MTANZANIA jana, Shilole alisema tangu afunge ndoa na mpenzi wake Uchebe, kumezagaa maneno ya majungu kitu ambacho hakiwezi kumkatisha tamaa na anaamini ndoa yake itadumu. “Mfa maji aishi kutapatapa, ndoa yangu imewaumiza wengi wasionipenda, nimeona maneno ya kashfa na majungu wakinichafua, sasa mimi nasonga mbele na maisha yangu sina habari na mtu,” alisema Shilole. Aliongeza kuwa familia yake imelipokea jambo hilo vizuri,…

Read More
Burudani 

Sababu ya Lulu kutopata Msamaha wa Rais Magufuli

Kuna watu wanajiuliza sana eti mbona Lulu msamaha haujamhusu, wanadhani kwamba misamaha huwa inatoka tu kiholela, hakuna kitu kama hicho usiumize kichwa saana kwa vitu vidogo ambavyo huwa vinafanywa kwa sheria maalum na wala si matakwa ya mtu husika. Misamaha yoote kuna vigezo ambapo kila mahakama kinatazama mwenendo wa mfungwa Tabia yake, aina ya kosa na urefu wa kosa kwa muda gani amesha tumikia kifungo chake, bahati mbaya sana Lulu hoko kote bado maaana hata mwezi hajamaliza. 648 total views, 648 views today The post Sababu ya Lulu kutopata Msamaha wa Rais…

Read More
Burudani 

Baada ya sakata la dawa za kulevya, Wema aweka wazi mahusiano yake na RC Makonda

Tangu mrembo Wema Sepetu akamatwe kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya kwa kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mnamo mwezi Februari mwaka huu, Mrembo huyo hajawahi kumposti wala kumzungumzia kwa lolote kama alivyokuwa akifanya hivyo kipindi cha nyuma. Watu wengi waliamini kuwa kitendo cha Wema Sepetu kutajwa na RC Makonda kwenye  orodha ya Wasanii waliotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya kuliondoa urafiki wao waliokuwa nao awali. Sasa, Wema Sepetu ameamua kuwaonesha mashabiki wake kuwa hayo yote yameshaisha na kwa sasa amerudisha yake ya urafiki na…

Read More
Burudani Kitaifa 

NMB yadhamini tamasha la Mtoto Day Out, watoto wapata nafasi ya kufungua akaunti

Benki ya NMB imedhamini msimu wa pili wa tamasha la watoto ‘Mtoto Day Out’ ambalo limekutanisha watoto kutoka maeneo mbalimbali lililofanyika katika ukumbi wa Msasani Beach Club uliopo Kawe jijini Dar es Salaam. Akizungumza kuhusu ufadhili wa NMB katika tamasha hilo, Kaimu Meneja Mwandamizi Amana na Huduma za Bima NMB, Stephen Adili, alisema wamethamini tamasha hilo ili kuwawezesha watoto kukutana pamoja kufurahi wakiwa pamoja na wazazi wao. “Sisi kama NMB tumekuwa tukitoa huduma bora kwa ajili ya watoto kwa muda mrefu, zaidi tulikuwa tunaangalia suala la fedha, baadae tukaona ni vyema…

Read More
Burudani Slideshow 

MFALME WA ROCK AFARIKI DUNIA

MARNES-LA-COQUETTE, UFARANSA MKONGWE wa muziki wa Rock na filamu nchini Ufaransa, Johnny Hallyday, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 74, baada ya kusumbuliwa na saratani ya mapafu. Kifo hicho kimetokea mapema jana na mke wake, Laeticia Hallyday, alikuwa wa kwanza kutoa taarifa hiyo kupitia mitandao ya kijamii. Staa huyo alitangaza kuwa anasumbuliwa na saratani tangu Machi mwaka huu na alianza kupatiwa matibabu lakini hali yake ilionekana kubadilika siku hadi siku. “Johnny Hallyday ametuacha, ninaweka wazi taarifa hii nikiwa siamini kichwani mwangu. Lakini huo ni ukweli kwamba mume wangu hayupo…

Read More
Burudani Slideshow 

LINAH HABADILI DINI SABABU YA MAPENZI

Na BRIGHITER MASAKI MSANII wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Linah Sanga ‘Linah’, amesema si sawa kubadili dini kwa sababu ya mapenzi. Akizungumza na MTANZANIA, Linah amesema hayo baada ya baba mtoto wake kuwa wa dini tofauti na yeye, hivyo amedai kama atabadili dini ni kwa sababu ya Mungu na si mapenzi. “Unajua kiimani hutakiwi kufanya vitu juu juu, hata ukibadilisha dini ni kwa sababu ya Mungu si kwa sababu ya mapenzi, kwa upande wangu sikutaka kufanya hivyo. “Kwa upande wa mume hawapo tayari mtoto wao abadili dini na hata kwetu pia…

Read More