You are here

Misri, Saudi Arabia na Bahrain kufunga anga zake kwa ndege za Qatar

Misri inafunga anga zake kwa ndege za Qatar katika mzozo wa kidiplomasia unaozidi kukua huku Saudi Arabia na Bahrain nazo zikitarajiwa kuchukua hatua kama hiyo leo Jumanne. Nchi kadha zimekata uhusiano na Qatar, baada ya kuishutumu kwa kuunga mkono ugaidi katika eneo la Ghuba. Raia wa Qatar nchini Bahrain, Saudi Arabia na Muungano wa Milki ya nchi za kiarabu wamepewa muda wa wiki mbili kuondoka. Qatar inakana kunga mkono wanamgambo na waziri wake wa mashauri ya nchi za kigeni ametaka kuwepo mazungumzo. Serikali ya nchi hiyo imesema kwamba mzozo huo…

Read More

Watanzania watatu wala shavu la kuwa maofisa waandamizi CAF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika {CAF} limewateua watanzania watatu kuwa maofisa waandamizi katika kusimamia mchezo wa Kundi A hapo kesho utakaowakutanisha Ghana na Gabon kwenye uwanja wa Port Gentil kwenye michuano ya Afcon U-17 Watanzania hao ni Mwesigwa Joas Selestine, ambaye atakuwa Kamishna wa mchezo huo, Frank John Komba kupewa nafasi ya mwamuzi msaidizi pamoja na Dk. Paul Gaspel Marealle kushika kitengo cha kitaalamu cha uchunguzi kwa wachezaji wanaotumia dawa za kusisimua misuli. Katika hatua nyingine, Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania {TFF} imewapongeza viongozi hao waliochaguliwa na CAF…

Read More

Rais Magufuli: Makonda wewe chapa kazi, hata mimi ninasemwa kwenye mitandao

Tofauti na kile ambacho watanzania wengi leo walikuwa wakitarajia kuona Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli akichukua uamuzi mgumu dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, mkuu huyo wa nchi amemuelezea Makonda kuchapa kazi. Makonda anakabiliwa na kashfa lukuki ikiwemo ile ya kudaiwa kughushi vyeti na kwamba jina lake halisi ni Daudi Bashite, kutumia vibaya madaraka yake ikiwemo tukio la juzi la kuvamia studio za Clouds Media Group akiwa na wanajeshi wenye silaha akilamizimisha kurushwa kwa kipindi na zingine. Tukio hilo limelaaniwa…

Read More

Trump afuta sheria ya Obama kuhusu walioamua kuegemea jinsia tofauti msalani

Rais wa Marekani Donald Trump amebatilisha agizo lililotolewa na mtangulizi wake Barack Obama lililowafaa wanafunzi walioamua kuegemea jinsia tofauti, ikulu ya White House imesema. Bw Obama alikuwa ameagiza shule za umma kuwakubali wanafunzi walioegemea jinsia tofauti na ya kuzaliwa nayo, watumie jinsia waliyokuwa wameikumbatia. Lakini wakosoaji wake walisema kwa kutoa agizo hilo, serikali ilikuwa imevuka mpaka, na kwamba agizo hilo lilitishia usiri na usalama wa wanafunzi. Barua iliyotumwa kwa shule nchini Marekani ilieleza mabadiliko hayo yaliyofanywa na Bw Trump, na pia kuongeza kwamba agizo la Obama lilikuwa limesababisha suitafahamu. Aidha,…

Read More

Mimi Mars asema haikuwa rahisi kupata shavu la kusaini kwenye label ya dada yake ‘Mdee Music’

Music Label ya ‘Mdee Music’ imemtambulisha rasmi msanii mpya Mimi Mars ambaye anatarajia kuachia ngoma yake ya kwanza Alhamisi hii. Mimi Mars ambaye pia ni mdogo wake Vanessa Mdee amedai kuwa haikuwa rahisi kusainiwa kwenye label hiyo mpya ya Dada yake, “Nimepitia vitu vingi sana mpaka yeye kukubali kunisaini,” Mimi Mars aliiambia XXL ya Clouds Fm  “Kwasababu nilikuwa nataka kuanza muziki kitambo kama miaka mitatu iliyopita hivi, lakini alikuwa ananiambia bado sijawa tayari kwenye mambo kama sauti na vitu kama hivyo. Kwahiyo nilikuwa na pitia mitihani mingi mpaka yeye amekuja…

Read More

Matokeo ya UEFA jumanne hii: Barcelona yashinda kufurukuta mbele ya PSG

aya ni matokeo ya mechi za ligi ya mabingwa wa Ulaya Uefa zilizo chezwa Jumanne, 14 Februari 2017, ikiwa ni raundi ya mtoano ya timu 16 kwa mechi za kwanza. Matokeo haya hapa chini ya mechi za Jumanne, 14 Februari 2017 Benfica 1 Borussia Dortmund 0 Paris Saint Germain 4 Barcelona 0 Leo Jumatano, 15 Februari 2017 inaendelea kwa gemu mbili Bayern Munich v Arsenal Real Madrid v Napoli Mwandishi: sadock kutoka TEAMTZ

Read More