You are here

RC wa Tanga awataka wakulima na wafugaji kuchukua mikopo katika benki ya NMB

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella,amewataka wakulima na wafugaji waliopo katika Kata ya Mkata Wilayani Handeni kutumia fursa ya mikopo inayotolewa na benki ya NMB ili waweze kuendeleza shughuli zao pamoja na kujikwamua kiuchumi. Shigella,alitoa wito huo juzi wakati akizungumza na wananchi wa kata hiyo katika hafla fupi ya ufunguzi wa tawi jipya la benki ya NMB lililopo katika Kata ya Mkata Wilayani Handeni Mkoani humu. Shigella, alisema kuwa kuwepo kwa benki hiyo katika eneo hilo itasaidia kuchochea uchumi na maendeleo ya Kata, Wilaya na hata Mkoa hivyo ni vyema wakulima, wafugaji na wafanyabiashara wakatumia…

Read More

Asasi za kiraia zaiomba Serikali kuboresha Sheria ya Usalama Barabarabi ya 1973

Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani umeiomba Serikali kuifanyia maboresho sheria ya Usalama barabarabi ya mwaka 1973 ili iweze kukabiliana ipasavyo na suala la ajali za barabarani pamoja na athari zinazotokana na ajali hizo. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga alipokuwa akisoma tamko la pamoja la asasi hizo katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani. “Pamoja na mambo mengine,…

Read More

Meli ya Hospitali kutoka China yawasili Dar, kuanza kutoa huduma Novemba 20

Meli kubwa ya Jeshi la Jamhuri ya China yenye hospitali (Chinese Hospital Ship) imewasili katika bandari ya Dar es Salaam ikiwa na madaktari bingwa 381, vifaa na madawa ya kutosha kwaajili ya kuanza kwa zoezi la upimaji na matibabu bure kwa wakazi wa Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametembelea Meli hiyo na kujionea namna imesheheni vifaa tiba vya kisasa ambapo ndani yake vipo vyumba 8 vya upasuaji, vyumba vya ICU, wodi za wagonjwa, vyumba vya madaktari, mitambo ya kisasa, maabara na sehemu ya…

Read More

RASMI Lazaro Nyalandu ajiunga Chadema

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amejiunga rasmi na chama cha CHADEMA leo katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani jijini Mwanza. Baada ya kukabidhiwa kadi ya Chadema, Nyalandu ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram,“NASIMAMA mbele yenu na mbele ya Watanzania wote nikiwa nimeisubiri kwa shauku kubwa siku hii ya leo ili nipate fursa ya KUJIUNGA na harakati za kupiganiq mageuzi ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi nchini Tanzania, kwa kujiunga Rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema. Asanteni sana kwa upendo wenu na…

Read More
Kitaifa Siasa Slideshow 

POLISI WATAWANYA KWA MABOMU WALIOTAKA KUMWONA LOWASSA

Upendo Mosha na Elizabeth Hombo -Kilimanjaro/SINGIDA JESHI la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, limelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya kundi kubwa la wananchi waliozuia msafara wa Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa. Maelfu ya wananchi hao walitawanywa jana kwa mabomu hayo baada ya kuziba barabara ya Soko la Mbuyuni eneo la Manyema wakati msafara wa Lowassa ukielekea Kata ya Bomambuzi, Manispaa ya Moshi. Akizungumza na gazeti hili, Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basili Lema, alisema polisi walilazimika kurusha…

Read More
Kitaifa Siasa Slideshow 

MAGUFULI, KAGAME, SI MADIKTETA – PROF. LUMUMBA

Na JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM MWANAZUONI maarufu barani Afrika, Profesa Patrick Lumumba, amesema Rais Dk. John Magufuli na Rais wa Rwanda, Paul Kagame si madikteta bali wanachokifanya ni kuhakikisha kunakuwa na siasa za miiko na maadili. Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana katika Mkutano wa Pan African Humanitarian wa mwaka huu ulioandaliwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (Yuna) uliokuwa na kaulimbiu ya “amani inawezekana jana, sasa na kesho” na kuwakutanisha vijana kujadili nafasi zao katika kuleta amani barani Afrika. Profesa Lumumba ambaye ni raia wa Kenya,…

Read More

“Tuna malengo ya kuwa na watumishi wa sekta ya afya laki 1.8″- Dkt. Ndugulile

Watumishi wa kada mbalimbali katika sekta ya afya bado wanahitajika nchini ili kuboresha huduma ya afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania ili kuifikisha nchi katika uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa mahafali ya pili ya chuo cha Afya na tiba cha KAM yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam. “Tuna malengo ya kuwa na watumishi wa kada mbalimbali za sekta ya afya wapatao laki 1.849 na kati ya hao tumefanikiwa kuajiri watumishi…

Read More

RC Dar atoa zawadi ya gari kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameagiza kukamatwa kwa madereva wote wanaovunja Sheria za Usalama Barabarani kwakuwa wamekuwa chanzo cha ajali. RC Makonda amesema hayo kwenye Uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambapo amewataka Askari wa Usalama kusimamie Sheria kikamilifu lakini wahakikishe hakuna uonevu. Katika uzinduzi huo Makonda amemzawadia gari ya kisasa aina ya Mingle5 Pickup aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Dar es Salaam Kamanda Awadhi Haji kama motisha kutokana na kazi kubwa na nzuri aliyoifanya katika kupunguza msongamano wa magari, ajali na…

Read More

Naibu Waziri wa Kilimo atoa siku saba kwa mrajisi wa vyama vya ushirika

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa leo Novemba 18, 2017 amemuagiza Mrajisi wa vyama vya ushirika kukamilisha haraka kazi ya uchunguzi kwenye Bodi za vyama vya ushirika vya Mkoa wa Mtwara ili kubaini sababu zilizopelekea kuuzwa kwa magunia kiholela. Alisema kuwa kumalizika kwa uchunguzi huo kutarahisisha kuchukuliwa haraka hatua kali za kisheria kwa wale wote watakaobainika kukiuka sheria No 17 ya vyama vya ushirika. Naibu waziri alitoa agizo hilo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara baada…

Read More