You are here
Makala Michezo Kimataifa 

TEVEZ ANASHINDWA KULINDA THAMANI YAKE CHINA

NA BADI MCHOMOLO DESEMBA 29 mwaka jana, nyota wa soka nchini Argentina, Carlos Tevez, alitikisa dunia baada ya kusajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha ndani ya klabu ya Shanghai Shenhua ya nchini China akitokea Boca Juniors. Mchezaji huyo alisaini mkataba wa kuitumikia Shanghai Shenhua kwa miaka miwili na mshahara wake kwa wiki ukitajwa kuwa pauni 615,000, ambazo ni sawa na 1,835,560,000 za kitanzania. Alisaini mkataba huo akiwa na umri wa miaka 32, wengi walishangaa huku wakiamini kwamba umri huo ni mkubwa sana hivyo hawezi kucheza soka kwa muda mrefu baadae,…

Read More
Michezo Kimataifa 

CONTE AWAONYA WAPINZANI WAO KWA  HAZARD

LONDON, ENGLAND KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte,  ameonesha imani yake kuhusu kiwango cha winga wake, Eden Hazard, kuongezeka licha ya kuanza vibaya  mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu. Hazard alikosa michezo ya mwanzo wa msimu baada ya kufanyiwa upasuaji  katika kifundo cha mguu lakini amerejea uwanjani baada ya kupona. Winga huyo mwenye umri wa miaka 26, alikuwa msaada mkubwa katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Newcastle United, akishinda mabao mawili. Lakini Conte anaamini kuna mambo mazuri makubwa yanakuja kutoka kwa wachezaji wake huku akimtaja Hazard kutumia…

Read More
Michezo Kimataifa 

MOURINHO AFICHUA ALIVYOICHINJA ARSENAL

LONDON, England JUZI kocha Arsene Wenger na vijana wake wa Arsenal walishindwa kuutumia uwanja wao wa nyumbani kwa kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Manchester United, mchezo uliokuwa wa 15 kwa kila timu tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi kuu. Mabao ya Man United katika mtanange huo yaliwekwa kimiani na Jesse Anthony, Valencia na Jesse Lingard aliyefunga mawili, huku lile la Gunners likipachikwa na straika wao raia wa Ufaransa, Alexandre Lacazette. Hata hivyo, kocha Jose Mourinho amefichua siri ya kikosi chake kuondoka na pointi tatu licha ya kuwa…

Read More
Michezo Kimataifa 

STERLING KULIPWA MIL. 650/- KWA WIKI

MANCHESTER, England MTANDAO wa Sun umefichua kuwa Manchester City wanaangalia uwezekano wa kumpa mkataba mpya winga, Raheem Sterling ambao utamfanya awe anavuna kitita cha pauni 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) kwa wiki. Hayo ni maelekezo ya Pep Guardiola ambaye anataka kuona mchezaji huyo akibaki kwenye kikosi hicho, hata kwa kiasi hicho cha fedha ambacho kitamfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mnono zaidi Ligi Kuu England. Kama mambo yatakwenda vizuri katika mazungumzo ya mkataba huo, basi Sterling mwenye umri wa miaka 22 atampiku hata staa wa Manchester United, Paul Pogba ambaye…

Read More
Michezo Michezo Kimataifa Slideshow 

SANTOS AZISIKITIKIA MOROCCO, IRAN KOMBE LA DUNIA

LISBON, Ureno KOCHA wa timu ya Taifa ya Ureno, Fernando Santo, amesema ni kikosi chake na Hispania ndicho kitakachofuzu hatua ya 16 bora ya fainali za mwakani za Kombe la Dunia na akaongeza kwamba, anazionea huruma Morocco na Iran. Kauli yake inakuja baada ya droo ya hatua ya makundi kuchezeshwa juzi jijini Moscow, Urusi, ambapo mataifa hayo manne yalipangwa Kundi B. Licha ya kusema anaziheshimu Morocco na Iran, Santos alisema ni ngumu kuziona timu hizo zikisonga mbele, ingawa zilikata tiketi ya kucheza fainali hizo za Urusi bila kufungwa katika michezo…

Read More
Michezo Michezo Kimataifa Slideshow 

KLOPP AIKIMBIA VITA YA SALAH, SUAREZ

MERSEYSIDE, England HUKU mashabiki wa soka, hasa wa Liverpool wakijiuliza ni mchezaji gani hatari zaidi kati ya Luis Suarez aliyeondoka na Mohamed Salah, kocha Jurgen Klopp amesema asihusishwe katika mjadala huo. Klopp amesema havutiwi na namna wachezaji hao wanavyofananishwa, akisema hiyo ni kazi ya magazeti na mitandao ya kijamii, hivyo haimhusu. Salah, raia wa Misri, amekuwa moto wa kuotea mbali tangu alipojiunga na Liver, kwani ameshaipachikia mabao 17 tangu kuanza kwa msimu huu, yakiwamo mawili aliyotupia Jumatano ya wiki hii katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stoke City. Makali…

Read More
Michezo Kimataifa Slideshow 

ROBINHO JELA MIAKA TISA KWA KUBAKA

MILAN, Italia MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester City na Real Madrid, Robson de Souza ‘Robinho’, amehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka msichana raia wa Albania Januari, 2013. Ripoti kutoka nchini Italia zinaeleza kwamba, Robinho, akiwa na wenzake watano, walihusishwa na kumvamia na kumbaka msichana huyo mwenye umri wa miaka 23 katika klabu ya usiku ya jijini Milan.Tukio hilo ambalo mchezaji huyo alisisitiza hakuwa sehemu hiyo, lilitokea wakati nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 akicheza timu ya AC Milan, baada ya kuondoka katika…

Read More
Michezo Kimataifa 

BAO LA POGBA ZAWADI KWA WATUMWA LIBYA

MANCHESTER, ENGLAND KUINGO wa mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Paul Pogba, baada ya juzi kufanikiwa kupachika bao lake la kwanza kwa kipindi cha miezi miwili, ametumia ukurasa wake wa Instagram kutoa zawadi ya bao hilo kwa watumwa nchini Libya. Pogba juzi alishuka dimbani kwa mara ya kwanza baada ya kukaa kwa miezi miwili akiwa majeruhi, hivyo aliweza kuifungia bao timu yake na kutoa pasi moja ya mwisho katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Newcastle kwenye Uwanja wa Old Trafford, katika michuano ya Ligi Kuu nchini England. Mchezaji huyo…

Read More
Michezo Kimataifa 

SERGIO RAMOS AVUNJIKA PUA

MADRID, HISPANIA NAHODHA wa klabu ya mabingwa watetezi wa klabu bingwa barani Ulaya, Real Madrid, Sergio Ramos, juzi alivunjika pua katika mchezo dhidi ya Atletico Madrid kwenye michuano ya Ligi Kuu nchini Hispania. Wapinzani hao walikutana kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo msimu huu na mchezo huo ulimalizika huku zikitoka bila ya kufungana kwenye Uwanja mpya wa Atletico Madrid, Wanda Metropolitano. Ramos ambaye alikuwa anaongoza safu ya ulinzi ya Real Madrid, alijikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya kuvunjika pua wakati anaokoa mpira wa hatari kwenye eneo la 18…

Read More
Michezo Kimataifa 

LEROY SANE MCHEZAJI BORA OKTOBA

MANCHESTER, ENGLAND KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Manchester City, Leroy Sane, amefanikiwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini England wa Oktoba, baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda michezo mitatu mfululizo mwezi huo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, amekuwa tegemeo kwenye kikosi cha kocha Pep Guardiola na amekuwa akipachika mabao mengi pamoja na kupiga pasi za mwisho katika michezo mbalimbali. Katika michezo mitatu ya Oktoba, ameweza kufunga kila mchezo na kutoa pasi ya mwisho. Kutokana na mabao sita aliyoyafunga mchezaji huyo na kutoa pasi tano za mwisho ndani…

Read More