Demi-Leigh Nel-Peters, Miss wa South Africa atwaa taji la Miss Universe 2017

Miss South Africa, Demi-Leigh Nel-Peters ametwaa taji la Miss Universe 2017. Nel-Peters amewashinda mshindi wa pili Miss Colombia Laura González na wa tatu Miss Jamaica Davina Bennett usiku wa Jumapili huko Las Vegas, Marekani. Nel-Peters, 22, hivi karibuni alipata shahada ya business management, North-West University. Walioingia wengine waliongia kwenye 13 bora ni kutoka Thailand, Sri Lanka, Ghana, Spain, Ireland, Croatia, Uingereza, Marekani, Brazil, Canada, Philippines, Venezuela na China. Mwandishi: sadock kutoka TEAMTZ

Read More