You are here
News 

BREAKING NEWZ Jaji Mstaafu wa mahakama Kuu, Upendo Msuya afariki dunia

Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ambaye amejiuzulu  hivi karibuni, Upendo Msuya amefariki leo Julai 19 baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kiharusi. Mjomba wa marehemu, Niva Mbaga amethibitisha tarifa hizi na kusema kwamba marehemu amefariki akiwa Hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa. Amesema kwamba shughuli za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es Salaam. “Amesumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kiharusi hivyo akawa anapelekwa hospitali na kurudi nyumbani zaidi ya miezi mitatu sasa na leo hii amefariki dunia’’ amesema Mbaga Amesema marehemu ameacha watoto wanne. The post…

Read More
News 

Serikali Yamjibu Tundu Lissu….Yadai ni Muongo, Mpotoshaji

Serikali imemshauri Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kutekeleza wajibu wake kwa kusimamia weledi akiwa kama Wakili wa Mahakama Kuu badala ya kufanya Propaganda kwa kutumia lugha ya kejeli, kuudhi na uchochezi kuituhumnu Serikali kuwa inabana demokrasia nchini. Hayo yameelezwa leo, Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi katika taarifa kwa Umma aliyoitoa juu ya ufafanuzi kuhusu propaganda na upotoshaji wa Mbunge huyo. “Vyombo mbalimbali vya habari leo vimemnukuu…

Read More
News 

Mahakama Yakataa Ombi la Kigogo wa Escrow Harbinder Singh Seth Kutibiwa Nje ya Nchi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekataa ombi la Mawakili wanaomtetea mfanyabiashara Harbinder Singh Seth la kumruhusu mteja wao kwenda nje ya nchi kutibiwa uvimbe uliopo tumboni na badala yake apatiwe tiba kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili. Wakili wa kujitegemea, Alex Balomi aliifahamisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana kuwa Harbinder Singh Sethi anaumwa, hali yake imeendelea kubadilika na hii  ni wiki ya nne sasa  hawezi kupata usingizi. Wakili Balomi aliiambia mahakama hiyo kuwa Sethi anasumbuliwa na uvimbe tumboni ambao unahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari. “Kutokana na hali yake kuwa…

Read More

Wagombea CCM Kibiti Washindwa Kuchukua Fomu….Kisa

Wakati hali ya wasiwasi ikizidi kushamiri kwa wakazi wa wilaya za Kibiti na Rufiji juu ya usalama wa maisha yao kutokana na kuendelea kwa matukio ya mauaji, hofu hiyo bado imetanda miongoni mwa wanachama wa CCM wanaohofia kuchukua fomu za kuwania uongozi ngazi ya matawi na shina. Akizungumza na gazeti la Mwananchi kwa njia ya simu, Katibu wa Siasa na Uenezi wa chama hicho katika wilaya hizo, Mussa Mnyeresa amesema sababu za wanachama kususa kuchukua fomu hizo hasa ngazi za tawi, shina na  nafasi nyingine ni mfululizo wa matukio ya…

Read More
News 

Rais Magufuli aizika rasmi BRN……Wafanyakazi wahamishiwa idara nyingine za Serikali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Juni, 2017 ameagana na wafanyakazi wa iliyokuwa Ofisi ya Rais, Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (President’s Delivery Bureau – PDB) ambao wamehamishiwa katika ofisi na taasisi nyingine za Serikali kwa ajili ya kuendelea na utumishi wa umma. Wafanyakazi hawa ndio walikuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN). Mhe. Rais Magufuli amekutana na wafanyakazi hao Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo amewashukuru kwa kazi nzuri waliyoifanya wakiwa PDB na…

Read More
News 

CHADEMA Waache Kabisa Kuwa Reactive Wawe Proactive Kama Awali Katika Siasa za nchi yetu

Kabla ya ujio wa Lowasa na kuondoka kwa Dr. Slaa, Chadema kilikuwa kinaongoza mijadala kuhusu mstakabali wa nchi yetu. Chadema walifanikiwa ku-plan strategically mijadala na mikakati ya kisiasa nchini na hivyo kuwafanya CCM kuwa katika defensive mode (kujihami). CCM kilipata ganzi ya akili na hivyo kazi yao ilikuwa kuwasubiri CDM waibue mijadala na hivyo CCM kuwa reactive. Mambo yaligeuka kabisa tangu helikopita ilipogiga reverse angani. That was a defining moment ambapo CDM ilianza kuwa reactive. Harakati za vijana wa CDM, ambao walikifanya chama kupendwa kwa hoja zao mruwa zikafifishwa. Akatangulizwa…

Read More
News 

KKKT Waliamsha DUDE…Wamtaka Rais Magufuli Akamilishe Katiba Mpya

ASKOFU mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville, amemuomba Rais Dk. John Magufuli kumalizia mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya ulioachwa na mtangulizi wake. Akizungumza baada ya kuwekwa wakfu Askofu Gaville na msaidizi wake, Himidi Sagga, katika ibada iliyofanyika juzi katika Viwanja vya Shule ya Msingi, Gangilonga, alisema Wakristo na Watanzania kwa ujumla wana imani kubwa na Serikali ya Dk. Magufuli na ni matarajio yao kwamba mchakato wa kuandika Katiba mpya utamalizwa kama lengo lilivyokuwa. Askofu huyo alisema Dayosisi ya Iringa inatoa mwaliko…

Read More