You are here

Wajumbe wapya Yanga wateuliwa

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga ameteuwa wajumbe wapya 12 watakaounda kamati ya mashindano. Katika wajumbe hao wapya waliyoteliwa, Magid Suleiman ameteuliwa kuwa Mwenyekiti na Mustapha Urungo kuwa Makamu Mwenyekiti. Mwandishi: sancho song kutoka TEAMTZ

Read More

Watanzania watatu wala shavu la kuwa maofisa waandamizi CAF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika {CAF} limewateua watanzania watatu kuwa maofisa waandamizi katika kusimamia mchezo wa Kundi A hapo kesho utakaowakutanisha Ghana na Gabon kwenye uwanja wa Port Gentil kwenye michuano ya Afcon U-17 Watanzania hao ni Mwesigwa Joas Selestine, ambaye atakuwa Kamishna wa mchezo huo, Frank John Komba kupewa nafasi ya mwamuzi msaidizi pamoja na Dk. Paul Gaspel Marealle kushika kitengo cha kitaalamu cha uchunguzi kwa wachezaji wanaotumia dawa za kusisimua misuli. Katika hatua nyingine, Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania {TFF} imewapongeza viongozi hao waliochaguliwa na CAF…

Read More

Man U wampa mkataba mpya Jesse Lingard

Mchezaji wa Manchester United Jesse Lingard amesaini mkataba mpya na timu yake na atakua akilipwa mshahara wa paundi 75,000 kwa wiki na kama timu yake watafuzu kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya atapata paundi 100,000 kwa Wiki. Mkataba wake huo mpya utabakisha Jesse klabuni hapo mpaka mwaka 2021 na kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka moja zaidi katika mkataba huo wa sasa. Lingard ameichezea klabu yake jumla ya michezo sabini, msimu huu amecheza michezo 29 na kufunga mabao 5 na alijiunga ma timu hiyo akiwa na umri wa miaka saba….

Read More

Mauricio Pochettino: Hata iweje siwezi kuwa kocha Barcelona

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amedokeza kwamba “haiwezekani” kwake kuwa meneja wa klabu ya Barcelona ya Uhispania. Mkufunzi huyo wa zamani wa klabu ya Espanyol alikutana na rais wa Barca Josep Maria Bartomeu wiki iliyopita huku uvumi ukiongezeka kwamba huenda akamrithi Luis Enrique. Hata hivyo, BBC imefahamu kwamba yeye si miongoni mwa wanaotathminiwa kwa ajili ya kupewa kazi hiyo. “Mimi ni shabiki wa Espanyol – Nafikiri sihitaji kusema sana kuhusu hilo,” raia huyo wa Argentina alisema, akisisitiza uhasama kati ya Espanyol na majirani zao wa jiji Barcelona. Pochettino, 45, pia…

Read More

FIFA yaidhinisha kuwepo timu 48 kombe la dunia

Chama cha soka duniani FIFA kimepanga kuwepo kwa michezo sita ili zipatikane timu zitakazoingia katika fainali za kombe la dunia mwaka 2020. FIFA imefafanua ni kwa namna gani timu 48 zitaweza kushiriki michuano hiyo. Rais wa shirikisho la soka Ulaya Aleksander Ceferin amesema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo na nchi za Ulaya zitawakilishwa vyema. Mchakato utakuaje? Kila mwanachama wa FIFA atakuwa na uwezo wa kuongeza walau timu moja katika michuano ya mwaka 2026. Mwenyeji wa fainali hizi ataingia moja kwa moja kama ilivyokua awali. Mapendekezo yapo hivi Afrika – 9…

Read More

Arsenal yasitisha mazungumzo kuhusu mkataba wa Ozili na Snachez

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema klabu hiyo imesitisha kwa muda mazungumzo kuhusu mikataba ya Alexis Sanchez na Mesut Ozil hadi mwisho wa msimu. Wenger amesema tayari amefanya uamuzi wake kuhusu mustakabali wake Arsenal, lakini bado hajatia saini mkataba wa miaka miwili aliopewa na klabu hiyo. “Kwa sasa hatujaafikiana,” Wenger aliwaambia BeIn Sports,  “Tumeamua kuangazia mwisho wa msimu na tuandae mazungumzo majira ya joto. “Hali ni sawa kwa Ozil, kwa sababu unapokosa kupata makubaliano na mashauriano bado yanaendelea, hilo si jambo jema, Ni vyema kuketi na kuiangazia majira ya joto.” Arsenal…

Read More

Kombe la Dunia 2018: Ratiba ya mechi za kufuzu bara la ulaya

Ijumaa hii ya Machi 24, Timu za bara la ulaya zitaanza mechi za kufuzu kombe la dunia  zitakazo fanyika nchini Urusi mwaka 2018. Mechi zitakazochezwa ni pamoja na michezo ya kundi D, ambapo Georgia watacheza na Serbia, Austria watakua wenyeji wa Moldova na Ireland wakicheza dhidi ya Wales. Huku kundi G Hispania watakipiga na Israel, Liechtenstein wao watapimana ubavu na Macedonia, timu ya taifa ya Italia itacheza dhidi ya Albania. Wakati huo huo Croatia wao watakua wenyeji wa Ukraine, huku Kosovo wakicheza na Iceland na Finland watakuwa ugenini dhidi ya Uturuki hii ikiwa ni…

Read More

Mke wa Michael Essien anunua kablu ya mpira wa miguu Italy

Mke wa aliyekuwa mchezaji wa Ghana Michael Essien ameinunua klabu ya ligi ya tatu Como ,kulingana na klabu hiyo. Akosua Puni Essien ameripotiwa kulipa pauni 206,000 katika mnada wa klabu hiyo iliofilisika. Mmiliki mpya na timu yake sasa ana mpangowa kuimarisha kikosi cha kwanza pamoja na ile timu ya vijana kukuwa. Wataweka juhudi za kuifanya kurudi katika Serie B na kukuza vipaji vya vijana waliomo. Puni Essien amejielezea kuwa mfanyibiashara ,mshauri, mtu anayependa kusaidia na mama wa watoto watatu. Como imeshiriki mara kadhaa katika ligi ya daraja la kwanza ya…

Read More