You are here

Millard Ayo

Millard Afrael Ayo

Millard Afrael Ayo, maarufu kama Millard Ayo ni radio presenter maarufu nchini Tanzania kwa website yake ya millardayo.com pamoja na vipindi vya Amplifaya na Top 20 Countdown katika kituo cha redio cha Clouds FM.

Akiwa mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wanne wa mzee Afrael Ayo (mmeru wa Akheri na mfanyabiashara) na Mary Ayo (mwalimu), Millard Ayo alizaliwa mnamo tarehe 26 Januari katika mkoa wa Arusha nchini Tanzania.

Tangu alipokuwa mtoto, alikuwa ni mwenye uelewa wa haraka wa mambo, ambao ulipelekea mama yake mzazi kumuanzisha masomo katika shule ya Patandi Primary School akiwa mdogo sana kiasi kwamba alimaliza darasa la saba na miaka 12 tofauti na watoto wengine ambao huanza shule na miaka 7 na kumaliza na miaka 14. Ayo alifanikiwa kuhitimu masomo ya kidato cha nne mnamo mwaka 2002 bado akiwa ni mwanafunzi mdogo kuliko wote darasani kwake.

Kutokana na upenzi na kuvutiwa kwake na ufundi wa kutengeneza satelitte dish, tv deck na radio, Millard alijiunga na Arusha College of Electronics katika kipindi alichokuwa akisubiria majibu ya mitihani yake.

Japokuwa mama yake mzazi alimshawishi aendelee na masomo ya A level, ingawa kwa shingo upande kwa sababu alikuwa na mipango mingine. Mjomba wake anayeitwa Gabriel alitokea kuwa mkombozi wake baada ya kumshawishi Mama Millard kumuacha Ayo afanye kile anachokipenda. Ndipo Ayo alipojiunga kusomea utangazaji na uandishi wa habari mwaka 2004 katika chuo cha East Africa Training Institute.

Na huo ndio ulikuwa mwanzo wa safari yake mpaka leo alipofikia kuwa mmoja wa watangazaji maarufu na wenye mafanikio makubwa hapa nchini. Mpaka sasa ni mmiliki wa tuzo mbalimbali zikiwemo; Mtangazaji bora 2006 kutoka Tanzania Radio Awards, Website bora 2012 kutoka Vodacom Tanzania na African Stars pamoja na tuzo ya YouTube Sub-Saharan Africa Creator Awards 2016 katika vipengele vya habari na siasa.

Ayo anaongoza vipindi katika kituo cha redio cha Clouds FM. Vipindi vyake ni mojawapo ya vipindi vinavyopendwa na kusikilizwa na watanzania wengi. Vipindi hivi ni;

  • Top 20 – ambacho kinacover nyimbo bora zilizohit wiki nzima
  • Amplifaya – hiki hurushwa kuanzia jumatatu mpaka Ijumaa.

Ukifuatilia profile za Millard Ayo katika mitandao ya kijamii, ni kati ya watanzania wachache wenye followers wengi Twitter, Instagram, Facebook pamoja na Youtube.

Twitter: Wafuasi zaidi ya 500,000

Millard Ayo Twitter

Instagram: Wafuasi zaidi ya 2,000,000

Millard Ayo Instagram

YouTube: Subscribers zaidi ya 300,000

Millard Ayo YouTube

Facebook: Watu zaidi ya 1,700,000 wanampenda na kumfata.

Kwa ufupi, huu ni uthibitisho tosha jinsi gani kijana huyu anavyotumia kipaji chake alichojaliwa na Mungu katika kushawishi, kuelimisha na kuburudisha watu.

Na huo si mwisho tu, kutokana na matumizi ya simu za smartphone kuongezeka watu wengi wanatumia muda mwingi katika simu zao, za smartphone hivyo pia Millard Ayo ametengeneza Millard Ayo App inayokupatia habari kama katika website yake. App hii inapatikana kwa ajili ya simu za Android pamoja na Apple. Kwa idadi ya smartphone/tablets ambazo Millard Ayo app imekuwa downloaded na installed ni kati ya 500,000 na 1,000,000 kwa mujibu wa Google Playstore.

 Millard Ayo App | LeoHub                         Millard Ayo App | LeoHub

Kati ya vitu vinavyozidi kumpa tuzo, mafanikio pamoja na umaarufu mtangazaji huyu miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ni uwezo wa kuwa wa kwanza katika kutoa taarifa za matukio yoyote yanotokea nchini. Kuanzia magazeti ya leo, habari mpya, matukio mapya, michezo mpaka matukio ya kijamii na kisiasa.

Ayo, mission yake ni kuhakikisha wafuasi wake hawapitwi na matukio katika nyanja mbalimbali yanayotokea ndani na nje ya nchi.